March 15, 2015

MAJI NI UHAI

Mazingira Plus
Maji ni Rasilimali muhimu si tu kwa binadam bali mimea, wanyama, ndege na hata wadudu. Wakati mwanadam anajishughulisha na hatua za maendeleo ya kiuchumi na kijamii hususan kwa zile shughuli zinazoambatana na matumizi ya vyanzo vya maji, huwa anasahau kabisa kuwa maji yanatumiwa na viumbe vingine tofauti.

Mathalani, kwa wanyama kama wale walio mbugani huwa wanakuwa katika wakati mgumu katika kipindi cha ukame, kwani hujikuta maji waliyozoea kuyakuta yakitiririka huwa ni haba. hivyo hupelekea mrundikano wa wanyama katika vidimbwi vichache vyenye maji, na hii husababishwa na matumizi ya maji hayo huambatana na matumizi makubwa kuanzia maeneo ambayo kuna chanzo cha maji, kati ya mto hadi unapomwaga baharini.

Suala hili hupelekea majanga na upotevu wa rasilimali wanyama pori kwa kufariki kwa kukosa maji kwa muda mrefu. hivyo basi husababisha upotevu wa wanyama hata wale walio katika hali ya upotevu (Endangered Species) kama vile Faru n.k

Aidha, suala lingine linalopelekea kukauka kwa vyanzo hivyo vya maji ni kutokana na athari za mabadiliko ya Tabianchi. hakika bila mikakati zaidi kuwekwa ili kukabiliana na athari hiyo, basi ni dhairi shairi tutashuhudia hali mbaya zaidi kwa kipindi cha miaka 20 ijayo hakuta kuwa na vita za mafuta bali kutakuwa na vita za maji.

Ni wakati wa kila mmoja sasa kupaza sauti ili kuchukua hatua stahiki ili kulinda na juhifadhi vyanzo vya maji, kwani maji ni uhai.

 Mabadiliko ni mimi, Wewe na Yule.
   

No comments:

Post a Comment