Licha ya Mkuu wa mkoa wa
Dar es salaam Said Meck Sadick kuwataka wananchi wanaoishi mabondeni
kuhama katika maeneo hayo kufuatia mvua zilizoanza kunyesha jijini Dar es
salaam wakazi hao wamegoma kuhama katika maeneo hayo.
Wakizungumza na Times FM hii leo
mara baada ya mvua kunyesha, wakazi hao wanaoishi maeneo ya mabondeni
yanayohusisha Bonde la mto Msimbazi, Jangwani pamoja na Msasani baadhi ya
wananchi wamesema kwamba wanashindwa kuhama katika maeneo hayo kutokana na
kutokuwa na kodi ya kulipia katika maeneo mengine yasiyo hatarishi.
Kwa mujibu wa Uchunguzi
uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa wakazi wanaoishi nyumba za mabondeni
hulipia chumba kwa kuanzia shilingi elfu kumi na tano hadi elfu ishirini kwa
mwezi. Yaani kwa upande wa elfu 15 kwa miezi sita hulipia elfu tisini
(90,000) na upande wa elfu ishirini hulipia shilingi laki moja na elfu
ishirini(120,000) kwa muda wa miezi sita.
Kwa upande wa nyumba zisizokuwa
katika maeneo ya mabondeni hulipia kiasi cha kuanzia elfu hamsini (50,000) kwa
mwezi ambayo ni sawa na shilingi laki tatu(300,000) kwa miezi sita.
Licha ya kodi kuwa bei ya chini
kwa nyumba za mabondeni sababu nyingine kubwa inayokwamisha wananchi hao
kuhama wamesema kwamba ni serikali kushindwa kuboresha miundombinu ya maji
taka yanayozalishwa katika maeneo ya mabondeni huku
ikiwalazimisha kuhamia mabwepande ambako wanadai kuwa hakuna huduma za
kijamii hadi sasa.
No comments:
Post a Comment